Saturday, November 16, 2013

BAADA YA FILAMU ZAO KUBUMA SOKONI...BONGO MUVI SASA WASHIKANA UCHAWI...!!

Tuhuma ya mastaa Bongo kujihusisha na mambo ya ulozi au uchawi imeibuliwa upya na safari hii bundi kajikita zaidi kwenye kiwanda cha sinema za Kibongo, Ijumaa lina ripoti kamili.

http://4.bp.blogspot.com/-6rq5Op4EJJk/TvHoS15grOI/AAAAAAAACVA/0DnQiFtM1BY/s1600/26.jpg
UCHUNGUZI
Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya ulimwengu wa mastaa hao ulibaini kwamba, ukiwaacha wale wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakishikana uchawi kila kukicha, kwenye filamu ndiko hakufai.

Ilibumburuka kwamba masuala ya kurogana ndiyo yamesababisha filamu za baadhi yao kudoda na kukosa soko.
Inaelezwa kwamba mbali na sinema  zao kubuma sokoni pia wamekuwa wakizibiana riziki za tenda kama ilivyokuwa zamani.

Elizabeth Michael 'Lulu'.
KIVIPI?
Kwa mujibu wa ‘mtaalam’ wao mwenye kituo cha kazi huko Yombo-Buza, Dar, wanachokifanya ni kufifisha na kuzimana nyota hivyo kumpotezea mhusika mvuto kwenye jamii.
“Unajua kuna mastaa ambao walikuwa na majina makubwa sana lakini siku hizi siyo kama zamani.

“Baadhi wanawaroga wenzao kwa kuwasababishia matatizo ya magonjwa au kwenye familia,” alisema mmoja wa wasanii waliokuwa waking’ara zamani lakini siku hizi kafifia huku akimtolea mfano mwigizaji mmoja wa kiume ambaye mkewe aliwahi kumkuta na hirizi.
Katika uchunguzi huo, baadhi ya mastaa walikuwa wakinyoosheana vidole wao kwa wao huku listi ndefu ya mastaa wanaokesha kwa waganga kuwamaliza wenzao ikianikwa (majina tunayo).
Ili kupata uthibitisho wa uchunguzi huo, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya vinara wa filamu za Kibongo ambapo wengi walikiri kukithiri kwa ushirikina kwenye tasnia hiyo.

JACOB STEVEN ‘JB’: Sanaa yoyote ili idumu muda mrefu inahitaji baraka na neema ya Mungu. Sisi tulianza enzi za Nyota Ensemble ‘Mambo Hayo’, baadaye ilikuja Kaole Sanaa Group ndipo kukaibuka mapinduzi sisi tukashuka.
Mimi siamini mambo ya uchawi ila naamini katika kazi tu, wasanii waache kufanya kazi kimazoea.

Masuala ya kurogana mimi spendi kuyapa nafasi maana hayo kila sehemu yapo, ninachoweza kusema ni kwamba wasanii wengi wa Bongo hawapo ‘siriasi’. JACQUELINE WOLPER: Mimi naamini sana katika kazi lakini kwa kuwa Mungu ndiye kanipa jina hili, sina budi kumshukuru yeye ila kama nimelipata kwa njia ya uganga basi nikose kabisa.
ROSE NDAUKA: Uchawi ni ishu inayonisikitisha sana na ukweli wapo mastaa wanafanya mambo hayo ili wapande. Mimi najua Mungu hawezi kuwasaidia so nawashauri wafanye kazi, wasihangaike na uchawi kwa sababu hauwezi kuwapandisha.
KAJALA MASANJA: Kusema kweli uchawi unatajwa sana kwenye tasnia ya filamu Bongo hadi inanifanya kuamini hivyo kwa sababu kuna watu kweli wakikuona unang’ara kwenye muvi watafanya kila wawezavyo ili wakushushe tu na hasa kwa njia ya ushirikina.
SINGLE MTAMBALIKE ‘RICHIE’: Mimi asili yangu ni Mwanza so kama ujuavyo watu wa Mwanza ni wachapa kazi, so nipo makini sana na kazi yangu ya filamu na nipo kwenye tasnia kwa miaka 17 na maisha yangu nayafanya ya kawaida tu wala sipendi kujikweza sana.
Kwa staili hiyo ningetumia nguvu za giza ningekuwa tajiri namba moja  hapa nchini maana siri ya kazi yoyote ni kuiheshimu na kujibidiisha. ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’: Tasnia yetu ya filamu naona kama hatuangalii mbali maana kwa wenzetu wanashindana kikazi na si uchawi kama huku wanaofikiria kuwashusha wenzao kisa wanaona wanafanya vyema, mimi ninachoweza kusema watu wafanye kazi na wasibaki kuangalia nani anafanya nini na kumfanyia mambo kama hayo yasiojenga maisha.
RUTH SUKA ‘MAINDA’: Mimi sijui sana kama kuna watu wanafanya ushirikina. Ninachowaomba wamtegemee sana Mungu kwani ninachoamini mimi kila kitu kipo kwa makusudi ya Mungu. Kama ukimroga mwenzio ili ashuke basi hata wewe huwezi kufika mbali.
JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’: Kweli mimi ninaumizwa sana na watu wanaotumia uchawi kuzima nyota yangu kwa sababu kweli wapo wanaofanya hivyo tunawaona hata huko lokesheni wanakamatwa na hirizi.
Wengine wanakutwa na matunguri ila mwisho wa siku naomba wajue kuwa nyota na mafanikio ya mtu huletwa na Mungu na kujibidisha katika kazi hivyo ninachoweza kuwashauri watu kama hao waachane na imani za kishirikina.
SALUM HAJI ‘MBOTO’: Mimi ninachojua watu wanatengeneza muvi kupitia migongo ya wenzao, unakuta mtu anatengeneza sinema lakini anajua kabisa bila kumchezesha fulani hawezi kuuza hivyo anatumia nyota ya mwenzake kuuza filamu yake.
AUNT EZEKIEL: Siamini sana katika kurogana ila wanotumia njia hizo siamini kama wanafanikiwa kiasi hicho maana uigizaji ni kipaji kutoka kwa Mungu na hakuna awezae kushusha kipaji hicho ila najua uchawi upo na watu wanatumia uchawi kwenye mambo yao.
STEVE NYERERE: Uchawi haupo kwenye filamu tu hayo yapo hata kwenye siasa. Watu kibao wanatembelea nyota za watu. Wapo wanaoshinda kwa waganga, tunawajua ila cha msingi wafahamu kuwa hata ukimfanyia mtu kitu gani huwezi kuwa staa.
SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’: Mimi ninaona kama chalenji tu na kinyongo, maana wengi wanaotumia nguvu za giza hawachukui muda mrefu wanashuka wao. Ninachoona mimi waachane na nguvu za giza wamtegemee Mungu.
Baadhi ya waigizaji wengine waliowahi kurogwa na wenzao ni pamoja na Wema Sepetu, Blandina Chagula ‘Johari’, Nuru Nassor ‘Nora’ na wengineo.

CREDIT: GPL
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © ZINDUNA | Powered by Blogger